Viongozi wa dini na wachambuzi wa masuala ya kisiasa mkoani Mtwara,wameipongeza tume ya taifa ya uchaguzi...
Viongozi wa dini na wachambuzi wa masuala ya kisiasa mkoani Mtwara,wameipongeza tume ya taifa ya uchaguzi kwa kuendesha kwa ufanisi uchaguzi mkuu, huku wakiitaka kutoyumbishwa na mashinikizo toka kwa viongozi wa vyama vya kisiasa katika utekelezaji wa majukumu yake.
Wakizungumza na ITV viongozi hao wa dini na wachambuzi wa siasa wamesema wanaipongeza tume kwa kuwa imeweza kuepusha vurugu za vyama kugombea maeneo ya kufanyia kampeni,kufuatia hatua yake kutoa ratiba ya mikutano ya kampeni mapema,imeweza kusambaza vifaa ya kupigia kura sehemu zinazohusika kwa wakati,pia kwa kuweka utaratibu wa kutangaza matokeo kwenye vituo, ambao umesaidia kuondoa dhana ya kuwepo uchakachuaji matokeo,mambo ambayo hayakufanyika kwenye chaguzi zilizopita,huku pia jeshi la polis likipongezwa kwa kusimamia amani.
Aidha wamemwomba rais ajae kutambua watanzania wengi ni maskini, na hivyo wamemtaka atumie vizuri rasilimali zilizopo nchini, kuwaondoa watanzania katika maisha hayo, na pia ajitahidi kurudisha upendo na mshikamano,ambayo umeathiriwa na kampeni za kuchafuana na hali ya ukanda iliyoanza kujitokeza.
Kwenye uchaguzi huo, mkoa wa mtwara wenye majimbo 9, ccm imefanikiwa kupata majimbo 4, cuf majimbo 2 na chadema jimbo 1, huku majimbo mawili ya lulindi na masasi hayakufanya uchaguzi, kwa lulindi haukujanyika kutokana na fomu kukosewa, wakati kwa jimbo la masasi, ni kutokana na kifo cha mgombea wa chama cha nld dr. Emanuel makaidi kufariki dunia.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni