Jeshi la Polisi limejipanga kuimarisha ulinzi maeneo yote nchini wakati wa uchaguzi...



Jeshi la Polisi limejipanga kikamilifu kuimarisha ulinzi katika maeneo yote nchini kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha kuwa taifa letu linapita salama katika kipindi hiki cha kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo ya uchaguzi.

Akizungumza na vyombo vya habari katika makao makuu ya jeshi la polisi nchini, mkuu wa jeshi hilo Inspecta Generali wa polisi Erenest Mangu amesema jeshi lake limejipanga kuimarisha ulinzi hivyo wananchi wasiwe na hofu bali wajitokeza kupiga kura ili kupata viongozi wanaowakubali.
 
Jeshi hilo limepiga marufuku uwepo wa mikusanyiko ya wafuasi wenye itikadi tofauti za kisiasa katika eneo moja sambamba na ubebaji wa bendera na hasa kwenye vyombo vya usafiri ili kuzuia vitendo vya uvunjifu wa amani.
 
Aidha mkuu wa jeshi la polisi nchini amesema kwamba jeshi lake litafanya kazi zake bila uonevu kwa chama chochote na kwamba wagombea wa vyama vya siasa wafuate sheria na makubaliano waliosaini kuhusu uchaguzi.










SOURCE:ITV









































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..