Ndege ya Urusi yenye abiria 200 yaanguka Sinai..
Ndege ya shirika moja la ndege la Urusi, iliyowabeba abiria zaidi ya 200, imeanguka katika eneo la Sinai nchini Misri, afisi ya waziri mkuu wa Misri imethibitisha.
Ndege hiyo aina ya Airbus A-321 ilikuwa imetoka mji wa Sharm el-Sheikh ikielekea mji wa St Petersburg nchini Urusi ilipoanguka.
Vyombo vya habari nchini Misri vinasema ambaki ya ndege hiyo yamepatikana na ambiulensi zaidi ya 20 zimetumwa eneo la ajali.
Awali, kulikuwepo na utata kuhusu hatima ya ndege hiyo, baadhi ya ripoti zikisema ilitoweka karibu na visiwa vya Cyprus. Lakini afisi ya Waziri Mkuu wa Misri Sharif Ismail imethibitisha kwamba ndege hiyo ilianguka katikati mwa eneo la Sinai.
Afisi hiyo imeongeza kuwa Bw Islmail ameunda kamati ya dharura ya kushughulikia ajali hiyo.
Wengi wa abiria walio kwenye ndege hiyo ni watalii kutoka Urusi.
Ndege hiyo ni ya shirika la ndege la Kogalymavia. Ripoti za karibuni zinasema ilikuwa imewabeba abiria 217 na wahudumu saba.
Shirika la Urusi linalosimamia safari za ndege Rosaviatsiya limesema ndege hiyo safari nambari 7K 9268 iliondoka Sharm el-Sheikh saa 06:51 saa za Moscow (0:351 GMT) na ilitarajiwa kuwasili uwanja wa ndege wa Pulkovo mjini St Petersburg saa 12:10.
Waliongeza kuwa ndege hiyo ilikosa kuwasiliana na wasimamizi wa safari za ndege Cyprus dakika 23 baada ya kupaa kama ilivyoratibiwa na ikatoweka kutoka kwenye mitambo ya rada.
Kituo maalum kmefunguliwa uwanja wa ndege wa Pulkovo kusaidia jamaa za abiria waliokuwa kwnnye ndege hiyo, shirika la habari la Tass limesema likinukuu maafisa wa jiji la St Petersburg.
SOURCE:BBC
Maoni
Chapisha Maoni