Vyombo vya habari vya IPP vyapongezwa kwa kuelimisha jamii.
Balozi wa Sweden hapa nchini Bi Katarina Rangnitt ameelezwa kufurahishwa kwake na utendaji mzuri wa kuelimisha wananchi juu masuala mbalimbali ya maendeleo unafanywa na vyomba vya habari vya utangazaji vya IPP ikiwemo ITV/Radio One.
Balozi huyo wa Sweden ametoa kauli hiyo mara baada ya kutembelea vyombo vya habari vya utangazaji vya IPP mikocheni jijini Dar es Salaam na kujionea mwenyewe jinsi utayarishaji na urushaji wa vipindi unavyofanywa na vyombo hivyokwa weledi mkubwa.
Akiwa na mwenyeji wake mkurugenzi mtendaji wa ITV na Radio One Joyce Mhavile na balozi huyo alipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya vituo hivi vya ITV RAdio One na Capital Radio na TV na kujione namna utayarishaji wa vipindi pamoja na ukusanyaji wa habari unavyofanywa katika kuhabarisha wasikilizaji na watazamaji.
Akitoa tathimini yake mara ziara yake balozi hiyo wa Sweden ametoa changamoto ya kuendelea kufanya vyema zaidi katika tansia ya habari hasa masuala ya uhuru wa demokrasia pamoja na kuwashauri watanzania kushiriki vyema katika uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu kwa amani na utulivu.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni