TFDA wateketeza shehena za dawa za binadamu zilizopita muda wake wamatumizi Mbeya...



Shehena ya dawa za binadamu ambazo zimekwisha na muda wake wa matumizi zenye thamani ya shilingi milioni 92 zimesalimishwa na wafanyabiashara mkoani Mbeya na kuteketezwa na mamlaka ya chakula na dawa ili kulinda afya za watumiaji.

Dawa hizo za binadamu zenye uzito wa zaidi ya tani 3 zimesalimishwa kwenye mamlaka ya chakula na dawa, TFDA, na wafanyabiashara maarufu wa dawa jijini Mbeya ambapo dawa hizo zimeteketezwa kwa kuchomwa moto kwenye tanuli la kiwanda cha saruji cha jijini Mbeya.
 
Aidha mkaguzi msadizi wa TFDA mkoa wa Mbeya, Yusto Wallece amesema kuwa kutokana na maelekezo ya baraza la usimamizi wa mazingira NEMC, dawa hizo hazikutakiwa kuteketezewa katika dampo kama ilivyozoeleka kwa kuwa zilihitaji joto kali ili ziweze kuharibika.
 
Baadhi ya wananchi ambao wameshuhudia zoezi hilo la uteketezaji, wamepongeza hatua ya wafanyabiashara kusalimisha dawa hizo kwa hiyari huku wakiwataka wauzaji wa dawa za binadamu kuwa waaminifu ili kulinda afya za watumiaji.












SOURCE:ITV





































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..