MKWASA,HEMED MOROCCO, WAISHUHUDIA AZAM IKITOA DOZI..(PICHAZ)
Kocha mkuu Charles Boniface Mkwasa (kulia) akiwa na kocha msaidizi Hemed Morocco (kushoto) akifatilia kwa karibu mchezo kati ya Azam vs JKT Ruvu
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa pamoja na msaidizi wake Hemed Morocco jana walikuwepo uwanjani kushuhudia mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya Azam dhidi ya JKT Ruvu uliochezwa kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha JKT Ruvu kilikuwa mwenyeji wa mhezo dhidi ya Azam FC.
Mkwasa alikuwepo uwanjani ili kushuhudia viwango vya wachezaji wa Azam ambao amewaita kwenye kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia nchini Urusi zitakazofanyika mwaka 2018.
Kikosi cha Azam FC kilichocheza dhidi ya JKT Ruvu
Stars itakutana na Algeria kwenye mchezo wa awali November 14 jijini Dar es Salaam kabla ya kurudiana kwenye mchezo wa pili siku tatu baadae nchini Algeria.
Geofrey Nyange ‘Kaburu’ alikuwepo pia kushuhudia mchezo huo.
Tayari mkwasa ameshatangaza kikosi cha wachezaji 28 ambao watasafiri kwenda kuweka kambi ya siku 11 nchini Oman kwa ajili ya maandalizi ya kuwawinda Algeria ‘Mbweha wa Jangwani’.
Shomari Kapombe akitolewa nje ya uwanja baada ya kuumia akiwa uwanjani.
Wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha taifa kutoka Azam FC na ambao walicheza kwenye mchezo wa Azam dhidi ya JKT Ruvu ni pamoja na Aishi Manula, Shomari Kapombe, Abubakar Salum, John Bocco, Farid Musa na Himid Mao.
Frank Domayo (aliyevaa kofia nyeusi) akiwa jukwaani akishuhudia mchezo kati ya Azam dhidi ya JKT Ruvu
SOURCE:Shaffih dauda.com
Maoni
Chapisha Maoni