Kuelekea uchaguzi watanzania wametakiwa kuendelea kuilinda amani ya nchi...
Watanzania wametakiwa kuendelea kuilinda amani ya nchi na kuepukana na uchochezi wa kufanya vurugu na maandamano wakati wa kupiga kura na kutangaza matokeo ya wagombea wa viti mbalimbali katika uchaguzi.
Akizungumza katika maombi maalumu ya kuombea amani taifa iliyoandaliwa na umoja wa madhehebu ya dini mkoani Geita mkuu wa mkoa wa Geita Bi.Fatma Mwasa amesema hakuna maendeleo bila amani hivyo kuwataka waumini wa dini zote kuheshimu sheria na taratibu za uchaguzi.
Naye kamanda wa polisi mkoa wa Geita ACP. Mponjoli Mwalusambo amesema jeshi la polisi litahakikisha linasimamia haki na sheria ili kuhakikisha amani inadumishwa.
Baadhi ya viongozi wa dini nao wamewata wakristo kuomba rehema kwa mungu na kuliweka taifa la Tanzania mikononi mwa mungu ili kuepuka vurugu na machafuko kama yanavyotokea nchi zingine kwakuwa tanzania ndio kimbilio la watu wenye uhitaji wa hifadhi salama.
Uchaguzi mkuu wa mwaka huu umetajwa kuwa na mvuto wa aina yake tofauti na miaka ya nyuma ambapo vijana na washabiki wa vyama vya siasa wengi wao wameonekana kuongozwa na mihemko hivyo wamekumbushwa kulinda utanzania wao zaidi kuliko itikadi za vyama.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni