Dr Magufuli amewatahadharisha viongozi wa halmashauri kuacha kukopa fedha katika mabenki...



Mpango wa kukopa fedha kutoka katika mabenki ya kibiashara unaofanywa na baadhi ya halmashauri nchini ili kulipa fidia za ardhi inayotwaliwa na halmashauri hizo kutoka kwa wananchi kwa lengo la kujenga makao makuu ya wilaya utasababisha hasara na mzigo kwa wananchi kwa siku zijazo kutokana na mabenki hayo kutoza riba kubwa lakini pia kutoa mwanya wa ufisadi na rushwa kwa baadhi ya watendaji wasio waaminifu.

Akimalizia ziara yake mkoani Geita katika maeneo ya Nyang`wale na Sengerema ya kusaka ridhaa kwa watanzania kuliongoza taifa mgombea urais wa chama cha mapinduzi Dr John Pombe Magufuli anawatahadharisha na kuwashauri viongozi na watendaji wa halmashauri hapa nchini kuachana na mpango wa kukopa fedha kutoka katika mabenki ya biasahara ili kulipa fidia ya ardhi inayotwaliwa kutoka kwa wananchi.
 
Dr John Pombe Magufuli ambaye amepata mapokezi ya kuvunja rekodi katika jimbo la Sengerea kama ilivyo katika maeneo mengine nchini kuonesha kukubalika kwake kwa wananchi kama kiongozi mkombozi wa kulisaidia taifa kupiga hatua za kimaendeleo mbele ambapo baadhi ya wanavyama wa vyama vingine Chadema na CUF vikiwemo mioyo yao ikaelemewa na upendo kwa Dr Magufuli na kuamua kurejea CCM na kuongeza kuwa katika serikali yake hayatafanyika maamuzi magumu bali maamuzi makini kwa faida ya nchi.
 
Baadhi ya wananchi nao wanawakumbusha watanzania wenzao kumchagua kiongozi mwadilifu na mchapa kazi kabla ya mkuu wa msafara wa kampeni za CCM Alhaji Abdalah Bulembo kuwataka watanzania kupiga kura na kisha kurudi majumbani kusubiri matokeo huku akielezea uhalali wa kufanya hivyo.
 
Akirejwea jijini Mwanza kutokea Sengerema mkoani Geita barabara za jiji hilo zikawa finyu kutokana na wingi wa watu waliojitokeza kumpokea kipenzi chao ambaye anatarajiwa kurejea Dar es Salaam jumanne ya October 21 kuendelea na mikutano ya kampeni katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam. 










SOURCE:ITV


























Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..